METHALI KATIKA USHAIRI WA SHAABAN ROBERT
Abstract
Makala haya yanaangazia matumizi ya methali katika ushairi wa Shaaban Robert. Kwa ambavyo methali ni zao la utamaduni wa jamii, matumizi yake yameuweka ushairi huo katika mkabala wa uhalisi wa maisha ya watu. Kupitia kwa methali, tungo za ushairi wa Kiswahili zinakuwa kanzi ya kuhifadhia na kubainishia falsafa ya mtunzi kuhusu maisha. Kadhalika, ujumbe unaowasilishwa hueleweka kwa tafakari kuhusu masuala mbalimbali katika jamii. Kwa maana hiyo, mtunzi amejenga dira ya kuwaelekeza wanajamii katika kukabiliana na matatizo katika jamii ya sasa. Aidha, methalikatika tungo za mshairi huyu zinajibainisha zaidi katika tamathali za usemi. Kutokana na namna zimetumiwa, ushairi wa Shaaban Robert unaweza kuanishwa kwa vijitanzu mahususi. Isitoshe, methali hizo zinawasilisha mawazo muhimu yanayothibitiwa kwa utamaduni wa jamii. Katika muktadha huo, ushairi wa Shaaban Robert umeshughulikia nyanja muhimu katika maisha ya watu. Tungo hizo zimekuwa zikienziwa siyo tu hapa Afrika Mashariki bali pia kutafsiriwa katika lugha muhimu za kimataifa na kutambuliwa ulimwenguni. Hii imetokana na kiwango cha juu katika ubunifu na udhibiti wa vipengele vya lugha viilivyotumika katika uwasilishaji wa maudhui. Kwa hivyo, ushairi wa Shaaban Robert umeweza kuweka msingi katika utunzi na uwasilishaji wa ushairi wa sasa wa Kiswahili.
Full Text:
PDFRefbacks
- There are currently no refbacks.