RUBAA ZA KIMAPENZI KATIKA BAADHI YA ETI ZA MASHAIRIYA SHAABAN ROBERT

M. S. Khatib

Abstract


Mapenzi huota katika mtima wa kila binadamu.  Mbegu yake husitawi na kushamiri kwa watu wa jinsi, kabila rika na dini tofauti. Mapenzi yalikuwapo tokea binadamu wa kwanza kutokea duniani. Kwa miaka nenda rudi, mapenzi yamekuwa yakiwasulubu na kuwaadhibu watu wasio na idadi. Wengine waliopewa uso na mapenzi, yamewanyanyua na kuwapa hadhi na heshima. Wengine kwa dahari, mapenzi yamewakumbatia na kuwapumbaza isivyo na kadiri. Mapenzi hayachaguwi wa kumshika kumkumbatia na kumwacha mkono. Hakuna asiyepigwa dafurao. Sio watawala si watawaliwa; si wakwasi si wachochele; si wasomi si wajinga.  Nani hajakumbwa na zilizala ya huba?  Hakuna.

Shaaban Robert (kuanzia sasa ‘Shaaban’) akiwa ni binadamu; isitoshe, ni mwamume shababi, aliyeishi katika jamii hakuweza kuyapiga chenga mapenzi. Angetaka asingethubutu.  Hakusalimika. Rubaa ya mapenzi imempiga dafrau. Shaaban akiwa mshairi kwa kupitia beti zake anabainisha jinsi mapenzi yalivyomtesa na kumfurahisha katika maisha yake.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.