Tathmini ya Nyimbo za Muziki wa Kizazi Kipya Karne ya 21 Nchini Tanzania: Tija na Madhara yake

Gervas A Kasiga

Abstract


 DOI: https://doi.org/10.56279/mulika.na42t1.5

 

Makala haya yamefanya tathmini ya nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa karne ya 21 nchini Tanzania. Makala yamechunguza tija na madhara ya muziki huu kwa wasanii na hadhira. Vigezo vya kibiashara na kidhamira viliteuliwa kushughulikia jambo hili. Kupitia tathmini, makala yamebaini kuwa katika karne ya 21 muziki wa kizazi kipya umeweza kufanikiwa kujenga mahusiano ya kifani na wasanii wa nje ya Tanzania. Pia, imebaini kuwa muziki huu unasisitiza uwepo wa mapenzi ya kweli katika jamii, unafariji, na kutia moyo kwa waliokata tamaa. Tija nyingine za muziki wa kizazi kipya zilizobainishwa ni uongezaji wa fursa za kiajira, utoaji wa elimu, na uburudishaji. Isitoshe, makala yamebaini madhara ya muziki huu yanayotokana na utumiaji wa lugha ya ufyosi, uhamasishaji wa vitendo vya ngono, na uhamasishaji wa kutumiwa mavazi yasiyofaa kwa hadhira. Vilevile, kufifisha nafasi ya nyimbo zenye kufuata maadili ya Kitanzania kusikilizwa na hadhira nalo limebainika kuwa ni suala linaloletwa na madhara ya muziki huu. Mwisho, imependekezwa kuwa ni vema kwa nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa karne ya 21 kuweka msisitizo zaidi katika masuala yanayoweza kujenga


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.