Matukio ya Mchakato wa Kujiua katika Riwaya ya Rosa Mistika
Abstract
Makala haya yanabainisha baadhi ya matukio ya mchakato wa kujiua yanayosawiriwa katika riwaya ya Rosa Mistika (1971). Lengo la kubainisha matukio hayo ni kuonesha kwamba kujiua si suala linalotokea ghafla, bali ni mchakato ambao huweza kuchukua muda mrefu kabla ya kitendo chenyewe kufanyika. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO, 2018) na gazeti la Habari Leo la Septemba 11 (2019), kujiua ni janga linalotokea kila siku duniani kote na linawaathiri watu wa mataifa, tamaduni, jinsi, dini, na matabaka yote. Data za uchunguzi huu zilipatikana kwa njia ya usomaji na uchambuzi makini wa riwaya ya Rosa Mistika. Kuteuliwa kwa riwaya hii kulitokana na taarifa za awali alizokuwa nazo mwandishi wa makala haya zinazohusu kujiua kwa mhusika mkuu, Rosa. Kwa msingi huo, riwaya hii iliteuliwa kama kiwakilishi cha riwaya nyingine zenye matukio ya kujiua kwa wahusika wake ili kubaini mchakato wa kujiua kwao. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Udhanaishi. Imebainika kuwa katika hali ya kawaida, kujiua huchukuliwa kama kitendo cha ghafla masikioni mwa watu. Hata hivyo, makala haya yamethibitisha kuwa kitendo hicho huwa hakimtokei mhusika kwa ghafla, bali ni mchakato ambao huambatana na matukio, mitanziko, na miktadha mbalimbali ya kimaisha. Hali hii inatokana na ukweli kwamba maisha ya binadamu ni sawa na kitendawili kigumu ambacho jibu lake si rahisi kulipata. Hivyo, kutokana na hilo, siku zote binadamu huyo huwa katika mchakato wa kutaka kutatua kitendawili hicho kwa sababu maisha kwake ni fumbo.
Full Text:
PDFRefbacks
- There are currently no refbacks.