Motifu ya Mawaidha katika Tawasifu ya Nasikia Sauti ya Mama (Ken Walibora)

Beth N. Mutugu

Abstract


Mtindo wa mtunzi una nafasi kubwa katika kuwasilisha maudhui ya kazi yake. Aghalabu, upekee wa mwandishi hudhihirika kutokana na matumizi ya vipengele mbalimbali vya kimtindo kama vile chuku, taswira, na motifu. Makala haya yanaangazia matumizi ya motifu ya mawaidha kama msingi mkuu wa tawasifu ya Nasikia Sauti ya Mama (2014) iliyoandikwa na Ken Walibora, mwandishi anayetambulika katika safu ya uandishi wa riwaya kwa namna anavyotumia mitindo teule ya utunzi inayoifanya kazi yake kuwa na mvuto. Kupitia tawasifu ya Nasikia Sauti ya Mama tunafahamu shida na changamoto mbalimbali alizopitia utotoni na ujanani na nafasi aliyochukua mama yake katika kumwelekeza na kumpa mawaidha kuhusu maisha. Mwandishi anatambua kuwa mama yake ndiye aliyekuwa nguzo ya maisha yake na kwamba mawaidha aliyopata yalimwezesha kufikia ngazi ya juu zaidi masomoni na katika maisha yake kwa ujumla. Isitoshe, ushauri alioupata ulimwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha. Mawaidha aliyopewa yanajitokeza kote katika tawasifu hii. Mawaidha hayo, yanaweza kutambulika kama motifu. Ni katika muktadha huu ambapo makala haya yamelenga kuangazia motifu ya mawaidha katika tawasifu hii.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.