Ujitokezaji wa Maudhui ya Utunzaji wa Mazingira katika Hadithi Teule za Watoto: Mifano kutoka Fasihi ya Kiswahili
Abstract
Ajenda ya utunzaji wa mazingira imetawala mijadala ya kitaifa na kimataifa. Baada ya kuanza kujitokeza kwa masuala ya kimazingira katika fasihi ya makundi mengine ya kijamii, fasihi ya watoto imebaki ikiwa imetengwa na kubaguliwa katika kushughulikia masuala hayo. Kwa hiyo, fasihi ya Kiswahili hususani utanzu wa fasihi ya watoto imejikuta ikipewa msisitizo usioridhisha na watunzi pamoja na wahakiki katika kuwasilisha na kuchambua masuala ya kiikolojia. Makala haya yanakusudia kushughulikia suala hilo kwa kuzingatia misingi mahususi ya Nadharia ya Uhakiki wa Kiikolojia. Uhakiki wa Kiikolojia ni nadharia inayochambua kazi za kifasihi kwa kujikita katika vipashio vya uhusiano au muumano na pengine utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Kwa mujibu wa nadharia hii, utamaduni wa jamii una nafasi kubwa ya kujenga mtazamo na mienendo inayoathiri matumizi ya mazingira kwa namna mbalimbali. Ili kutimiza lengo la makala haya, tumechambua data kutoka hadithi teule za watoto zilizobuniwa na kuandikwa katika muktadha wa fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania. Tumeanza kwa kutoa utangulizi, kufasili dhana ya mtoto, kuelezea misingi ya nadharia iliyotumika na kisha kuwasilisha data pamoja na uchambuzi wake.
Full Text:
PDFRefbacks
- There are currently no refbacks.