Taswira za Hali na Maana katika Nyimbo za Kizazi Kipya: Kundi la Offside Trick
Abstract
Makala hii inachunguza matumizi ya taswira za hali katika nyimbo za kizazi kipya, tukiangazia kikundi mahususi cha Offside Trick na maana mbalimbali zinazowasilishwa kupitia taswira hizo. Nyimbo za kundi hili zimechaguliwa kwa sababu aghalabu huwasilishwa kwa lugha yenye kujenga taswira za aina mbalimbali. Taswira tunazolenga kuchunguza ni zile ambazo hutumikisha hisia tano za mwanadamu; yaani zinazomfanya msikilizaji asikize, aone, anuse, aonje au aguse. Hivyo, taswira zitakazobainika katika nyimbo hizi zitachanganuliwa katika makundi matano kwa mujibu wa hali inayotumikishwa. Hivyo, taswira za usikivu zitawekwa katika kundi moja na kuchanganuliwa. Vivyo hivyo, taswira za mwono, za mnuso, za mwonjo na za mguso. Mbali na kuchunguza kutumikishwa kwa hali tulizozitaja, tutachunguza maana na ujumbe unaowasilishwa na taswira hizi kwa kizazi kipya, ambacho ndicho hadhira lengwa ya nyimbo hizi za Offside Trick. Utafiti huu utaongozwa na Nadharia ya Umaumbo kwa mujibu wa Viktor Shklovsky. Nadharia hii inasisitiza suala la ugeni katika kazi za fasihi kutiliwa maanani. Hii ni kwa sababu kuna tofauti kati ya lugha ya kawaida yenye lengo la kupasha tu ujumbe na lugha ya kifasihi kwa kuwa hutegua uzoefu wetu wa kuyaona na kuyaelewa mambo.
Full Text:
PDFRefbacks
- There are currently no refbacks.