Utata wa Maudhui ya Kisarufi katika Vitabu vya Kiada vya Kiswahili Kidato cha Kwanza na cha Tatu Nchini Tanzania

Alcheraus R Mushumbwa

Abstract


Vitabu vya kiada ni nyenzo muhimu katika ufundishaji wa somo la Kiswahili nchini Tanzania. Hutumika kama mwongozo wa ufundishaji wa mada zilizoteuliwa kwa kiwango husika cha elimu. Kutokana na umuhimu huo, vitabu hivyo huandikwa vizuri na kwa mpangilio mzuri wenye mantiki na unaoeleweka. Inapotokea kitabu cha kiada kimekuwa na changamoto za maudhui, kuna uwezekano wa maarifa yaliyokusudiwa kutowafikia walengwa kama inavyotakiwa. Hivyo basi, malengo ya makala hii ni kuchambua utata wa kimaudhui unaojitokeza kwenye vipengele vya mada za sarufi katika vitabu vya kiada vya Kiswahili (kidato I na III) na kupendekeza utatuzi wake kwa ajili ya maboresho zaidi. Data za makala hii zimepatikana kwa mbinu ya usomaji makini wa vitabu teule vilivyoandikwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kuwapo kwa utata kwenye baadhi ya vipengele vya sarufi katika vitabu hivyo. Baadhi ya utata uliobainika unahusu fasili za dhana, mifano iliyotolewa na ufafanuzi wa kushadidia hoja zilizomo vitabuni. Makala inapendekeza kuwa vitabu husika vinapaswa kupitiwa tena ili kurekebisha maudhui yanayoibua utata uliobainishwa.

https://dx.doi.org/10.4314/kcl.v21i1.4


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.