Majina Sadfa ya Wahusika katika Kusadikika na Kichwamaji

Lustina Kyando

Abstract


Mwandishi wa kazi za fasihi ni jicho la jamii hivyo anatumia sanaa yake ya utunzi kiubunifu zaidi katika kuyaeleza yale yanayoikumba jamii yake. Moja ya mbinu za kiubunifu anazotumia mwandishi wa fasihi ya Kiswahili ni matumizi ya majina ya sadfa. Mada hii imelenga kutafiti na kujua ni kwa nini mwandishi wa fasihi anatumia majina ya sadfa, jinsi majina hayo yanavyoteuliwa kwa ujumla, njia zinazotumika kuunda majina hayo, na faida na hasara za kutumia majina ya sadfa katika kazi za fasihi ya Kiswahili. Vitabu viwili vya fasihi ya Kiswahili vilivyotumika kutafiti mada hii ni Kusadikika (1981) na Kichwamaji (1974). Halikadhalika, vitabu vingine vitarejelewa hapa na pale, hususani Uhuru wa Watumwa (Mbotela, 1956), Ukiwa (Mkangi, 1975), Kiu (Mohamed, 1985, Nyuso za Mwanamke (Mohamed, 2010), Nagona (Kezilahabi, 1990), Kitumbua Kimeingia Mchanga (Mohamed, 2000), Rosa Mistika (Kezilahabi, 1980), na Gamba la Nyoka (Kezilahabi, 1979). Riwaya hizi zimeteuliwa kwa sababu zinasadifu mada husika inayofanyiwa utafiti hasa kuhusu kipengele cha majina sadfa ya wahusika.


Full Text:

pdf

Refbacks

  • There are currently no refbacks.