USAWIRI WA MASUALA IBUKA KATIKA FASIHI YA WATOTO: MIFANO KUTOKA KENYA

Dkt. Pamela M.Y. N Ngugi

Abstract


Fasihi ni zao la wakati katika jamii; jinsi jamii inavyobadilika ndivyo fasihi inavobadilika ili iweze kuyamulika masuala mapya yanayoibuka katika jamii husika kama vile, haki za binadamu, usawa katika jamii, madawa ya kulevya na mengine mengi. Kwa kuzingatia dhana ya hadithi-matini, makala hii imelenga kubainisha jinsi masuala ibuka yanajitokeza katika fasihi ya Kiswahili kwa watoto kwa lengo la kubainisha nafasi ya matini haya kama chombo cha kujenga uelewa na ufahamu kuhusiana na masuala ya kijamii.. Makala yatarejelea baadhi ya hadithi zilizoandikwa na waandishi mbalimbali kutoka Kenya.


Full Text:

pdf

Refbacks

  • There are currently no refbacks.