Mbinu za Ujenzi wa Wahusika na Usawiri wa Sifa Zao: Uhakiki wa Riwaya ya Dunia Uwanja Wa Fujo ya E. Kezilahabi
Abstract
Kipengele cha wahusika ni muhimu katika kuunda kazi yoyote ya kifasihi. Kipengele hiki hushirikiana na vipengele vingine vya kifani katika kutoa maudhui ya kazi yoyote ya kifasihi. Kwa kawaida wahusika hujengwa kisanaa na mwandishi ili waweze kuwakilisha dhana mbalimbali za maisha katika jamii (Msokile 1992). Mwandishi huwajenga wahusika wake kwa kutumia mbinu mbalimbali ili kuwatofautisha na hivyo kuiwezesha hadhira yake kutambua sifa au tabia za mhusika fulani zinazomtofautisha na mhusika mwingine katika kazi husika. Hata hivyo, ni vema ifahamike kuwa kila msanii wa kazi ya kifasihi ana mbinu zake za kuwajenga wahusika wake. Hii ina maana kuwa, msanii wa kazi ya kifasihi anaweza kutumia mbinu moja au zaidi katika kazi fulani kutegemeana na aina ya utanzu anaoushughulikia. Kwa kutambua hoja hiyo, makala haya yanafafanua mbinu mbalimbali zilizotumiwa na E. Kezilahabi katika kuwajenga wahusika katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo na mchango wa kila mbinu katika kubaini sifa za wahusika pamoja na dhamira katika kazi hiyo.Makala hii imegawanyika katika sehemu nne. Sehemu ya kwanza ni utangulizi unaotoa muhtasari kuhusu riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo; sehemu ya pili inazungumzia dhana ya wahusika katika fasihi; sehemu ya tatu inajadili mbinu mbalimbali zinazotumika kuwajenga wahusika na jinsi sifa za wahusika zinavyosawiriwa kupitia mbinu hizo; na sehemu ya nne ni hitimisho la mjadala katika makala hii.
Full Text:
pdfRefbacks
- There are currently no refbacks.