Raha na Karaha ya Uradidi wa Vitabu vya Fasihi kwa Shule za Sekondari Nchini Tanzania

Newaje Ali Mganga

Abstract


Mihtasari ya vidato vya tatu hadi sita kupitia ujuzi wa jumla na malengo ya ufundishaji wa somo la Kiswahili kwa shule za sekondari nchini Tanzania, imetoa mwongozo murua kuhusu utekelezaji wake. Kwa upande wa sarufi, mambo yamenyooka si haba, kwani mwalimu ana fursa ya kutoa mifano kulingana na mazingira ya darasa lake. Changamoto inayojitokeza ni katika upande wa mada za fasihi, kwani kuna mazoea ya kujirudiarudia kwa matumizi ya vitabu vya kibunilizi: diwani, riwaya na tamthiliya, licha ya kuwapo kwa vitabu vya kutosha katika uwanja huo. Suala hilo husababisha raha na karaha katika mustakabali wa wahitimu watarajiwa. Hivyo, makala haya yamenuia kudadisi raha na karaha hizo katika ustawi wa fasihi ya Kiswahili katika jamii. Ikumbukwe kwamba wanafunzi wa leo ndio wanafasihi wa kesho katika kuzitunga, kuzihakiki na kuzichambua kazi mbalimbali za fasihi ya Kiswahili. Kuandaliwa mazingira mazuri katika kujifunzi kutawezesha kupata wahitimu wenye uwezo wa kuhimili na kuhudumu nafasi hizo kwa weledi na uaminifu.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.