Athari za Mgawanyo Tofauti wa Majukumu ya Kijinsia katika Nyimbo za Watoto kwa Watoto
Abstract
Makala haya yanahusu athari za mgawanyo tofauti wa majukumu ya kijinsia katika nyimbo za watoto kwa watoto. Makala yameangazia zaidi kubaini majukumu ya kijinsia na namna yalivyogawanywa na kisha kuchambua athari zinazoweza kujitokeza kwa watoto kutokana na mgawanyo huo. Kwa mujibu wa mgawanyo huo tuna maoni kwamba kuna athari chanya na hasi zinazojitokeza kwa watoto wanaozitumia nyimbo hizi. Kwa kuzingatia uwiano wa mgawanyo huo kwa watoto, watoto wa kike huathiriwa zaidi kwa upande hasi kuliko watoto wa kiume. Fasihi ya watoto kwa ujumla na nyimbo za watoto zikiwamo kwa upande mmoja na suala la jinsia kwa upande mwingine ni mambo yanayohitaji utafiti zaidi kutokana na umuhimu wake katika kuwaandaa watoto ili wawe na msingi thabiti wa kutekeleza majukumu mbalimbali kulingana na uwezo wa mtoto na sio kwa kuzingatia jinsi ya mtoto. Carlson na wenzake (2004) wana hoja kwamba ubaguzi wa majukumu wa muda mrefu unawaathiri sana watoto katika hatua ya ujana. Vilevile, huo ni umri ambao msingi wa majukumu ya kijinsia hujengwa na kuimarika. Data za makala haya zilikusanywa kutoka katika shule za awali na shule za msingi hadi darasa la nne katika jiji la Dar es Salaam. Mbinu ya ukusanyaji wa data iliyotumika ni ushuhudiaji wa kushiriki.
Full Text:
PDFRefbacks
- There are currently no refbacks.