Malumbano ya Mchongoano: Je, Huchongoa au Kudumaza Watoto Kielimu na Kimaadili?
Abstract
Malumbano ya utani ni kijipera muhimu ndani ya kipera cha mazungumzo katika utanzu wa fasihi simulizi. Utani katika jamii nyingi za Kiafrika ni tukio la mazungumzo lililosheheni vichekesho ambavyo aghalabu hutumiwa kufurahisha na kusisimua jamii. Tangu azali, fani hii ya utani imekuwa ikitumiwa kuburudisha, kuchekesha, kuelimisha, kuadilisha na kuadibu jamii kupitia kwa malumbano yaliyosheheni ucheshi.
Katika jamii ya leo, hususan miongoni mwa watoto nchini Kenya, malumbano ya aina hii yamechukua sura na miundo tofauti. Hali hii inatokana na mifanyiko ya kijamii inayopaliliwa na kurutubishwa na teknolojia pevu za mawasiliano kupitia kwa msimbo wa Sheng. Aidha, malumbano hayo sasa hujulikana kama ‘Mchongoano’ na huundwa na kusambazwa kwa kasi na kizazi kipya cha watoto na hata vijana. Ubunifu huu wa kimtagusano umeendelea kusambaa hasa katika miaka ya hivi karibuni na hupatikana kwa wingi sasa katika mitandao ya kijamii.
Makala haya yanapigia darubini usuli wa mchongoano, sifa zake pamoja na athari za matumizi yake kielimu na kimaadili miongoni mwa watoto hususan nchini KenyaFull Text:
PDFRefbacks
- There are currently no refbacks.