Dosari za Kisarufi katika Maandishi ya Kiswahili Sanifu ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Nchini Burundi
Abstract
Utafiti huu ulichunguza utamalaki wa dosari za kisarufi zinazofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kwenye vyuo vikuu vya Burundi. Uchunguzi huu uliozingatia matini za kimaandishi ulifanyika kwa kutumia Nadharia ya Uchanganuzi Makosa (UM) ya Corder (1967) ambayo imeboreshwa na wanaisimu wa siku za karibuni kama Gass na Selinker (2008), Mahmoodzadeh (2012) na Al-khreshen (2015) ili kuchunguza na kutathmini makosa. Sampuli ya wanafunzi mia moja (100) ilitumika na data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchunguzi matini. Matokeo ya uchunguzi huu yamedhihirisha jumla ya dosari za kisarufi 981 zilizogawanyika katika aina nne ambazo ni: (a) dosari za kifonolojia kwa kiasi cha 37.2%, (b) dosari za kimaumbo kwa kiasi cha 21.8%, (c) dosari za kisintaksia na kimofosintakisia kwa kiasi cha 30.1%, na (d) dosari za kimsamiati 10.9%. Viwango vya utamalaki wa dosari katika matumizi ya kimaandishi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Burundi hasa ya kifonolojia na kimofosintaksia vimedhihirisha kuwa kunahitajika hatua za haraka za uboreshaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, walimu na mbinu thabiti katika ufundishaji wa somo la Kiswahili.
http://doi.org/10.56279/jk.v86i2.1
Full Text:
Subscribers OnlyRefbacks
- There are currently no refbacks.