Miaka 60 ya Ufundishaji wa Kiswahili nchini China
Abstract
Kozi ya Kiswahili ilianza kufundishwa nchini China tangu mwaka 1960. Katika miaka 60 iliyopita, kozi hiyo imepitia kipindi cha ukuaji (1960-1977), kipindi cha mdororo (1978-1999) na kipindi cha upanuzi (2000-Sasa) pamoja na mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi ya ndani pamoja na uhusiano baina ya China na Tanzania. Makala hii imepitia historia ya ufudishaji wa Kiswahili nchini China kwa ujumla. Pia, imehakiki maendeleo na changamoto zake katika masomo, vitabu vya kiada, walimu na wanafunzi na kutoa mapendekezo ya kuukuza ufundishaji na utafiti wa lugha hii nchini China.
Full Text:
Subscribers OnlyRefbacks
- There are currently no refbacks.