Mtazamo Linganishi wa Muundo na Maudhui ya Tenzi Mbili za Kale na Ushairi wa Muyaka
Abstract
Fasihi huelezea kuhusu matukio katika jamii. Kazi hizi huweza kuiga miundo, mitindo na maudhui ya kazi za awali. Kuiga huku huweza kufanya kazi hizo kuwa na vipengele vinavyofanana na kazi zilizotangulia. Kwa sababu hii, makala haya yanalenga kulinganisha miundo na maudhui ya tenzi mbili za kale za lugha ya Kiswahili na ushairi wa Muyaka Bin Haji. Tenzi hizi ni: Utendi Al-Inkishafi na Utenzi wa Liyongo. Uchanganuzi huu utaonesha ikiwa kuna sifa za kimuundo na kimaudhui zinazofanana katika tenzi hizi na pia kutofautiana, hasa ikizingatiwa kuwa watunzi wa tenzi hizi walitunga katika kipindi kimoja na Muyaka Bin Haji. Nadharia iliyoongoza uchanganuzi huu ni nadharia ya “Ukae” (Classicism) ambayo ina mihimili kama ukale wa msamiati, ubunifu wa kiwango cha juu, kurejelewa na wasanii wengine katika enzi tofauti kati ya mingine.
Full Text:
Subscribers OnlyRefbacks
- There are currently no refbacks.