Dhana ya Lafudhi katika Isimu: Mifano kutoka Lugha ya Kiswahili na Lugha Nyingine za Kibantu

Michael A. Mashauri

Abstract


Makala hii inalenga kuitalii dhana ya lafudhi kama inavyotumika katika isimu na kujaribu kuongeza kile ambacho hakijagusiwa na wanaisimu waliotangulia ambao walijishughulisha kwa namna moja ama nyingine kuiandikia dhana hii. Wataalamu wengi wemeizungumzia dhana ya lafudhi na kuitolea mifano ya tofauti za kivitamkwa pekee bila kuhusisha vipengele vingine ambavyo pia vinahusika katika kuitambulisha lafudhi ya mzungumzaji wa lugha fulani au wa mahali fulani. Makala hii inajaribu kuubainisha undani wa dhana ya lafudhi kuwa haihusishi vitamkwa tu bali pia vipengele vingine vya kimatamshi. Mifano iliyotumika inatoka kwa wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili sanifu, Kibena, Kifipa, Kihaya na Kinyamwezi. Aidha, mifano mingine kutoka katika lugha ya Kiswahili inatokana na utamkaji wa maneno ya Kiswahili kwa kutumia lafudhi ya Kiarabu kutoka kwa wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili walioathiriwa na utamkaji wa lugha ya Kiarabu.


Full Text:

pdf

Refbacks