Itikadi na Ufundishaji wa Nadharia za Uhakiki wa Fasihi

Richard Makhanu Wafula

Abstract


Ufundishaji wa nadharia za uhakiki wa fasihi ulipoanza, ilifikiriwa kwamba hatimaye fasihi imefanikiwa kupata silaha za kiuhakiki na kiakademia za kutegemewa. Wahakiki na wananadharia wa Kimagharibi kama Wellek na Warren (1986) walifikiria kwamba nadharia ya uhakiki wa fasihi ilikuwa moja popote fasihi iliposomwa. Hivi sasa katika Karne ya 21, nadharia ni nyingi na zinaendelea kuundwa kuendana na mazingira anuwai ambamo wahakiki wanapatikana. Makala hii inanuia kuonesha kwamba wingi wa nadharia zilizopo unaashiria uchimuzi wa itikadi zinazoratibisha kuwapo kwa nadharia hizo. Japo Wellek na Warren walikuwa wakizungumzia kuhusu nadharia katika umoja wake, walikuwa wakiitikia masuala ya kiitikadi. Jambo hili linahusu fasihi ya Kiswahili vilevile.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.