Uhakiki wa Nadharia ya Fomula ya Kisimulizi katika Tamthilia ya Jogoo Kijijini

Sophie Okwena

Abstract


Makala hii imehakiki Nadharia ya Fomula ya Kisimulizi katika tamthilia ya Jogoo Kijijini (1976). Tamthilia ya Jogoo Kijijini imewasilishwa katika muundo wa fasihi simulizi. Waaidha, tamthilia hii imechota malighafi yake kutoka Afrika. Katika tamthilia hii ya kidrama, Ebrahim Hussein ametumia muundo wa kitendawili, ngano na shairi huru, ambavyo ni baadhi ya vipengele vya fasihi simulizi ya Kiafrika katika utunzi wake. Licha ya kwamba watafiti waliotangulia walihakiki tamthilia hii kwa kuegemea katika wahusika, maudhui na mtindo; suala la nadharia iliyotumika katika utunzi wa tamthilia hii halijashughulikiwa kwa kina. Hivyo basi, kulikuwa na haja ya kuchunguza matumizi ya Nadharia ya Fomula ya Kisimulizi katika tamthilia teule. Uchunguzi huu umeongozwa na Nadharia ya Fomula ya Kisimulizi. Azma ya kutaka kubainisha fomula za uwasilishaji ndiyo imechochea matumizi ya Nadharia ya Fomula ya Kisimulizi kwa lengo la kuziba pengo lililopo. Uhakiki huu umefanywa kwa lengo la kuchanganua Nadharia ya Fomula ya Kisimulizi katika tamthilia ya Jogoo Kijiini. Kimsingi, uhakiki huu umedhamiria kuthibitisha kuwa Nadharia ya Fomula ya Kisimulizi imetumika katika utunzi wa tamthilia ya Jogoo Kijijini.


Full Text:

PDF

Refbacks

  • There are currently no refbacks.