“Nani Aliamua?” Sera ya Lugha na Kitokeacho Mahakamani Tanzania
Abstract
Makala hii inatazama ugumu wa lugha ya sheria na jinsi utekelezaji wa sera ya lugha ya mahakama nchini Tanzania unavyoweza kuathiri juhudi za kutenda haki. Makala imetumia dhamira mbili kati ya tatu za nadharia ya Symbolic Interaction, yaani ‘umuhimu wa maana kwa tabia ya binadamu’, na ‘umuhimu wa kuijenga nafsi kutokana na wenzetu watuonavyo’. Data iliyotumika imetoka kwenye kesi mbili za jinai, na matokeo yanaonyesha kwamba sera ya lugha ya mahakama na mapungufu binafsi huchangia kupunguza ufanisi wa maafisa wa mahakama. Mwenendo uliopo unaweza kuathiri vibaya mtazamo wa jamii kwa mahakama.
Dhana za msingi: lugha ya sheria, stenokalikimu, Symbolic Interaction, sera ya lugha ya mahakama
Full Text:
PDFRefbacks
- There are currently no refbacks.
[ISSN 0856-9965 (Print)]