TABIA ZA VITENZI VYA MJONGEO KATIKA LUGHA YA RUNYAMBO

Johari Hakimu

Abstract


Vitenzi vya mjongeo ni vile ambavyo vinaonyesha hali ya mjongeo. Mjongeo ni hali ya kitu kimoja kutembea, kuruka, kutambaa, kusogea n.k. kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Vitenzi vya mjongeo ndivyo hasa vinavyoonesha kitendo cha mjongeo, hali ya mjongeo na namna mjongeo unavyotokea (Bleam na Wenzie (Haina mwaka)). Lengo la makala haya ni kuchunguza vitenzi vya mjongeo katika lugha ya Runyambo ili kubaini tabia za vitenzi hivyo. Hata hivyo, si lengo la makala haya kutafuta upya katika vitenzi vya mjongeo ambao haupo katika vitenzi vingine vya Runyambo bali ni kutaka kuziba pengo la kitaaluma lililopo katika uwanja wa vitenzi vya Runyambo kwani Rugemalila (2005) ameshughulikia vitenzi vya Runyambo kwa ujumla bila kuangalia undani wa vitenzi vya mjongeo katika upekee wake. Hata hivyo, katika makala haya tumebaini ughairi wa baadhi ya vitenzi ambavyo katika shina lake vitenzi hivi vinaonekana si kamilifu kimaana mpaka viongezewe viambishi vingine. Vitenzi vya namna hii pamoja na vingine vimebainishwa na kujadiliwa katika makala haya.


Full Text:

pdf

Refbacks

  • There are currently no refbacks.